Wakati Manispaa ya Mtwara-Mikindani ikiwa kwenye mchakato wa kupitisha mapendekezo ya mpango na bajeti ya halmashauri kwa mwaka wa fedha wa 2023/224 katika vikao mbalimbali, Wajumbe wa baraza la wafanyakazi Manispaa ya Mtwara-Mikindani wameridhia na kupitisha makadirio ya mapato na matumizi yenye thamani ya shilingi bilioni thelathini milioni mia moja thelathini na mbili laki mbili sabini na moja mia nne na tatu (30,132,271,403).
Pamoja na Kupitisha mpango huo baraza hilo pia limepitia taarifa ya mapitio ya mpango na bajeti ya mwaka 2021/2022 ambapo Manispaa ya Mtwara-Mikindani iliidhinishiwa kukusanya na kutumia shilingi Bilioni 29,934,362,104 na ikafanikiwa kukusanya shilingi bilioni ishirini na tatu milioni mia mbili sabini laki tisa sabini na moja, mia tatu tisini na moja na senti sabini na tatu (23,270,971,391.73) sawa na asilimia 75.7
Aidha baraza hilo pia limepitia utekelezaji wa mpango na bajeti kwa kipindi cha nusu mwaka Kuanzia Julai 2022 hadi Desemba 2023 ambapo Manispaa ya Mtwara-Mikindani iliidhinishiwa kukusanya shilingi bilioni thelathini milioni mia moja thelathini na mbili laki mbili sabini na moja mia tano na sita (30,132,271,506) na hadi kufikia Desemba 2022 Manispaa imekusanya shilingi bilioni moja milioni mia tisa thelathini na sita laki nane arobaini na nane mia sita sitini na moja na senti themanini(1,936,848,661.80) sawa na asilimia 36.
Kikao cha baraza la wafanyakazi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kimefanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mtwara-Ufundi leo Januari 26, 2023.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.