Baraza la Wafanyakazi la Manispaa ya Mtwara-Mikindani limepitisha rasimu ya mpango wa Bajeti jumla ya Shilingi bilioni thelathini na tatu, Milioni Mia Tano Arobaini na Nne Laki Tisa Sabini na Moja Mia Nne na Sita elfu (33,544,971,406) kwa mwaka fedha 2025/2026.
Akizungumza katika Mkutano huo uliofanyika jana (Februari 25,2024) kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mtwara Ufundi, Mkurugenzi wa hiyo, Mwalimu Hassan Nyange amewataka wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi kujikita katika kuwasilisha changamoto za watumishi ili ziweze kufanyiwa kazi.
Aidha amelitaka Baraza hilo lisaidie kutoa mawazo katika kukusanya mapato huku akisisitiza kuendelea kuboresha maisha ya watumishi ikiwemo kulipa madeni mbambali na stahiki zao.
“Natamani kuwa na Baraza la wafanyakazi lenye maono ya mbali zaidi, tunapodhani kuwa kuna mambo ya msingi ya Halmashauri tusisubiri vikao vya kisheria,” alisema Mwalimu Nyange
Naye Katibu wa Baraza la Wafanyakazi, Bi.Sofia Malandi amewataka wajumbe wa Baraza hilo kuwasilisha changamoto za watumishi mapema ili zifanyiwe kazi badala ya kusubiri vikao vya kisheria ili baraza hilo liweze kuwa bora kuliko mabaraza yote ya Mkoa wa Mtwara .
Aidha akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa Baraza, Bi. Malandi amemshukuru Mkurugenzi wa Manispaa Mwalimu Hassan Nyange kwa kutatua changamoto za watumishi kutoka katika idara na vitengo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.