Katika kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Manispaa ya Mtwara-Mikindani kupitia mpango wake wa msitiri mtoto asome ,benki ya NBC tawi la Mtwara limekabidhi taulo za kike (pads)box 11 zenye thamani ya shilingi 220,000 kwa Mkurugenzi wa Manispaa ili aweze kuzigawa kwa wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya taulo hizo iliyofanyika Juni 1,2018 katika ofisi za manispaa Meneja wa benki amesema kuwa wao wameguswa na tatizo linalowakabili watoto hao la kutohudhuria masomo shuleni wanapoingia kwenye siku zao kutokana na ukosefu taulo za kike. Ameongeza kuwa wanaamini uwepo wa taulo hizo utasaidia watoto hao kuhudhuria masono yao vizuri nakuahidi kuendelea kushirikiana na manispaa katika kulisukuma gurumu la maendelo
Nae Asha Moto balozi wa mpango wa msitiri mtoto asome amesema kuwa kutokana na takwimu zilizofanyika zinaonesha kuwa wanafunzi wengi wanashindwa kuhudhuria darasani wakiwa kwenye siku zao hivyo yeye kama balozi amezungumza na wadau mbalimbali ikwemo benki ya Nbc ili kuunga mkono mpango huo na kusambaza taulo hizo kwa wanafunzi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa Bi Beatrice Dominic ameishukuru benki ya NBC na balozi wa mpango huo kwa kuanza kuchangia na kuwataka wadau wengine watakaoguswa kuunga mkono jittihada zilizofanywa na Manispaa kwa kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili wahudhurie darasani. Kama wenzao .
Juliana Manyama ,Afisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa amesema kuwa Mpango wa msitiri mtoto asome umeanzishwa baada ya wataalamu kufanya utafiti na kubaini kuwa wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu kwa siku 60 kwa mwaka hawahudhurii darasani hasa wanapo ingia kwenye siku zao kutokana na ukosefu wa taulo za kike na kusababisha kushuka kielimu.
Amesema kuwa ili kukabiliana na tatizo hilo Manispaa ikaanzisha mpango huo kwa kushirikiana na balozi wa mpango bi Asha Moto, wadau mbalimbali na wanajamaii ili kusaidia upatikanaji wa taulo hizo na kuzigawa kwa watoto wetu. Hata hivyo amesema kuwa ili mpango huo uwe endelevu ni vema kila mmoja akaliunga mkono jambo hilo ili kuwapatia watoto haki ya elimu kama watoto wengine.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.