Mwishoni mwa juma Benki kuu ya Tanzania tawi la Mtwara Pamoja na wanawake wa Benki hiyo walikabidhi msaada wa unga wa sembe kilo 775 pamoja na sukari kilo 60 kwa lengo la kuwasaidia wazee 54 wenye uhitaji ndani ya Manispaa Mtwara – Mikandani.
Mkuregenzi wa Benki hiyo tawi la Mtwara, Nassor Omar, alisema msaada hu oni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake wa BOT wao wakotoa kilo 250 na kufanya jumla ya kilo 775, Pamoja na sukari kilo 60.
Akiokea msaada huo kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Gwakisa Mwasyeba alishukuru Benki hiyo na kuahidi kuwa utatumika kwa lengo lililokusudiwa.
Aliongeza kuwa wanufaika wa msaada huo ni wazee 54 wenye uhitaji kutoka kata zote 18 za Manispaa hiyo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.