Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius byakanwa amewataka wazazi na walezi wa watoto wenye mahitaji maalumu(walemavu) kuacha mila potofu za kuwaficha watoto ndani badala yake wajtokze kwenye zoezi la utambuzi wa watoto hao ili wapate haki zao za kimsingi ikiwemo elimu.
Byakanwa ametoa wito huo Januari 11,2021 alipozindua zoezi maalumu la utambuzi wa watoto wenye mahitaji maalumu lililofanyika Kimkoa katika Shule ya Msingi Tandika iliyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Zoezi la utambuzi wa watoto limezinduliwa leo na litafanyika kwa siku kumi na nne katika halmashauri zote tisa zilizopo Mkoa wa Mtwara na linatarajia kuwatambua watoto wapatao 1259
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.