*Yaagiza Wananchi kuchangia Nguvu kazi katika Utekelezaji wa Ujenzi wa Nyumba za Watumishi Mbae na Mjimwema.
Mweyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mtwara Mhe. Yusufu Namnila ameridhishwa na maendeleo ya miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
“Nimerizishwa na maendeleo ya miradi inayotekelezwa, japo kuna changamoto kama mbili tatu lakini maendeleo ni mazuri na yanaleta hamasa” Amesema Mhe. Namnila
Mhe. Mwenyekiti ametoa pongezi hizo 20 Agosti, 2021 katika kikao cha majumuisho ya ziara ya Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ilipotembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Manispaa yetu.
Amesema kuwa kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo inaridhisha hivyo amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani COL. Emanuel Mwaigobeko, kuongeza kasi zaidi ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati na wananchi wanufaike na miradi hiyo.
Katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha miundombinu ndani ya Manispaa yetu, Mhe. Mwenyekiti amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kuhamasisha wananchi ili waweze kuchangia nguvu kazi katika ujenzi wa nyumba za watumishi hasa katika shule ya Msingi Mbae na Mjimwema.
Aidha ameitaka Mamlaka ya Maji safi na Salama Mkoa wa Mtwara (MTUWASA) kuhakikisha inashughulikia changamoto ya maji katika shule ya Msingi mbae, na kurekebisha bili ya maji katika zahanati ya Mbawala Chini.
“Haiwezekani bili ikiwa 800,000 kwa mwezi wakati hakuna matumizi makubwa hapa, bili haiendani na uhalisia wa matumizi nataka mfatilie na mrekebishe”
Miradi iliyotembelewa na Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mtwara ni pamoja na jengo la mionzi katika Kituo cha Afya likombe, ujenzi wa Zahanati ya Mbawala Chini, ujenzi wa madarasa 2 na matundu 11 ya choo Shule ya Msingi Mbae ,ujenzi wa madarasa 4 Shule ya Msingi Mjimwema,ujenzi wa Chujio la maji Mangamba pamoja na upanuzi wa uwanja wa ndege.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.