Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mtwara ikiongozwa na Mwenyekiti wake Ndugu Said Nyengedi Julai 3, 2023 imefanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya inayojengwa mtaa wa Mjimwema na kuridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo.
Pamoja na kuridhishwa na ujenzi huo Mwenyekiti wa Chama hiko Mkoa wa Mtwara Saidi Nyengendi ameitaka Manispaa kuhakikisha inajenga nyumba za watumishi kwenye hospitali hiyo ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa haraka pale inapotokea dharura.
Hospitali ya Wilaya ya Mjimwema inajengwa kwa gharama ya Shilingi Milioni mia tano (500,000,000) fedha za awamu ya kwanza ambazo zimetolewa na Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kuhudumia wagonjwa wa nje (OPD), maabara na kichomea taka.
Ujenzi wa hospitali hiyo unalenga kuimarisha utoaji wa huduma bora za afya ndani ya Manispaa, kusogeza upatikanaji wa huduma za afya, lishe na za ustawi wa jamii karibu na wananchi pamoja na kupunguza idadi ya vifo vya akina mama wajawazito, Watoto wachanga na waatoto walio na umri wa chini ya miaka mtano.
Aidha ujenzi huo kwa sasa upo kwenye hatua ya ufungaji wa Lenta na mradi unatarajia kukamilika ifikapo Septemba 30, 2023.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.