Chama Cha Mapinduzi (CCM) Manispaa ya Mtwara-Mikindani imeshinda ushindi wa kishindo kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kupata Wenyeviti wa Serikali za Mitaa yote 111 sawa na asilimia 100 kati ya Wenyeviti 228 kutoka vyama mbalimbali waliogombea nafasi hiyo.
Aidha Katika Nafasi ya Ujumbe Mchanganyiko Chama hicho kimepata wajumbe 333 katika viti 333 viliivyokuwa vinagombewa na jumla ya Wajumbe 514, sawa na asilimia 100 ya ushindi.
Kwa upande wa nafasi ya Ujumbe wa kundi la Wanawake CCM kimepata jumla ya wagombea 221 kati ya nafasi 222 ya wagombea 344 waliogombea sawa na asilimia 99.55.
Msimamizi wa Uchaguzi Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mwalimu Hassani Nyange amewashukuru wananchi kwa kufanya uchaguzi wenye amani na utulivu.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hapa nchini umefanyika Jumatano, Novemba 27, 2024 ukiwa na Kauli Mbiu inayosema “Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi”.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.