Ikiwa Leo April 22,2024 Tanzania imezinduanzoezi shirikishi la utoaji wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kw awasichana wenyeumrinunaoanzia miaka 9 hadi miaka 14 , Naibu Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mhe. Sixmund Lungu ametoa rai kwa wasichana wenye umri huo kujitokeza kwa wingi kw ajili ya kupata chanjo huku akiwatoa hofu ya usalama wa chanjo hiyo.
'Zoezi hili la utoaji wa chanjo linafanyika Tanzania nzima, Chanjo hii ni salama n haina amdhara kw amatumizi ya mwanadamu, msiwe na wasiwasi kwani zimefanyiwa uchunguzi wa kutosha "amesema mhe. Lungu.
Mhe Lungu ameyasema hayo kwneye uzinduzi wa wa chanjohiyo uliofanyikakatikaviwanja vya shule ya Sekondari ya Rahaleo.
Aidha amewataka walimu wa Shule zote za Msingi na Sekondari kuw amabalozi wakubwa wa kuwaelimisha wasicahna hao ili waweze kupata chanjo hiyo muhimu na walengwa wote waweze kufikiwa.
Akiongea kwa naiba ya Mkurugenzi wa Mnaispaa ya Mtwara-Mikindani Nicholuos Milanzi ametoa rai kw awazazi na walezi kuwaruhusu watoto wakapate chanjo ya sartani ya mlango wa kizazi ili kumkinga mtoto dhidi ya ugonjwa huo.
Zoezi la Utoaji wa hanjo ya Saratani ya Mlango wa kizazi Limezinduliwa Leo April 22,2024 na litakamilika April 28,2024 ambapo halamshauri ya Manispaa ya Mtwara-mikindani inatarajia kuchanja wasicahan wapatao 10,051
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.