Timu ya wasimamizi wa huduma za Afya [CHMT] ya Manispaa ya Mtwara- Mikindani ikipata mafunzo elekezi ya mfumo wa kiektroniki wa GOT-HOMIS ili kuwezesha vituo vya afya na zahanati kutoa huduma kwa ufanisi.
Mafunzo hayo ya siku mbili yameanza leo februari 23 na yanatarajia kuhitimishwa februari 24 katika ukumbi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani yakilenga kuwajengea uwezo na kuwarahisishia Timu ya CHMT kufanya ufuatiliaji wa mapato na utunzaji kumbukumbu katika vituo vya afya na zahanati.
Katika mafunzo hayo Mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwa pamoja na mfumo wa taarifa za maabara, uwekaji wa mfumo sahihi wa matumizi ya dawa, utozaji na ukusanyaji wa mapato ya dawa pamoja na kutunza kumbukumbu za afya za mgonjwa.
Katika kuhakikisha kuwa mapato kwenye vituo vya afya na zahanati yanakusanywa vizuri, Manispaa ya Mtwara-Mikindani imeshafunga mfumo wa GoT-HOMIS kwenye vituo vya afya na zahanati zote (Vituo vya afya 2 na zahanati 5) na kwa sasa mfumo huo unafanya kazi kwenye vituo vyote.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.