Timu ya Menejimenti (CMT) ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani leo Novemba 20, 2024 imefanya ziara ya kutembelea Miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri hiyo kupitia fedha kutoka Serikali Kuu na wahisani.
Ikiongozwa na Mkuu wa Idara ya Uratibu na Mipango, Ndg. Gwakisa Mwasyeba, kamati hiyo imetembelea miradi yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 60.2/- lengo ikiwa ni kujenga uelewa wa pamoja katika kusimamia miradi husika.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Mwalimu Hassan Nyange, Mwasyeba alisema kuwa ziara hiyo ni moja ya utaratibu waliojiwekea wa kila mwezi kutembelea miradi ya maendeleo kwa pamoja na kubaini changamoto mbalimbali wakati wa utekelezaji na kuzitatua kwa wakati.
Aidha, aliwasisitiza mafundi wote kuhakikisha wanaongeza kasi ya ujenzi ili miradi ikamilike ndani ya muda uliopangwa.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, Ndugu Alphonce Mulima, amewataka mafundi kuzingatia ubora wa majengo na thamani ya fedha huku akiwataka wasimamizi wa miradi kuwasimia kwa ukaribu mafundi hao kulingana na mikataba.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Ujenzi wa vyumba viwili (2) vya madarasa na matundu sita (6) ya choo Shule ya Msingi Magomeni, Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya (Mjimwema), Ujenzi wa Nyumba ya Mtumishi (mbili kwa moja) Shule ya Sekondari ya Mkanaledi, pamoja na Ukamilishaji wa Bweni la wanafunzi Shule ya Sekondari Naliendele.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.