Timu ya Menejimenti ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani leo Januari 13,2025 imefanya ziara ya Kutembelea Miradi mbalimbali ya Maendeleo inayoendelea kutekelezwa kwa kutumia fedha za mapato ya ndani ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na katika ubora unaokubalika
Aidha timu hiyo imewaagiza mafundi kufanya kazi kwa ufanisi kulingana na matakwa ya mradi na kwa kuzingatia mikataba waliyoingia na Halmashauri.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Ujenzi wa Jengo la Kuhudumia wagonjwa wa nje Zahanati ya Mtawanya (100,000,000), Ujenzi wa matundu kumi ya vyoo shule ya Msingi Chuno (20,000,000), Ujenzi wa Hospitali ya Mjimwema Bilioni 2.5, utengezaji wa viti na meza za wanafunzi 143 Shule ya Sekondari ya Chuno na Viti, meza na makabati .... Shule ya Sekondari ya Mangamba.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.