Timu ya Menejimenti ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani ikiongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Mwalimu Hassan Nyange imefanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miradi inayotarajiwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru tarehe 25.05.2025 Leo April 9,2025.
Mkurugenzi amewasisitiza wahandisi, mafundi na wasimamizi wa miradi kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana ili miradi iweze kukamilika kwa wakati na katika ubora unaotakiwa ili thamani ya fedha zilizotolewa ziweze kuonekana.
Aidha Timu hiyo pia ilitembelea Kata ya Naliendele katika Mtaa wa PWANI A kwa ajili ya kuangalia korongo lililotokana na maji ya mvua na ni hatarishi kwenye makazi ya watu Manispaa iweze kuona namna Bora ya kufanya kuhusu eneo hilo
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Tandika, Ujenzi wa Jengo la kuhudumia wagonjwa wa nje Zahanati ya Mtawanya, Ujenzi wa Jengo la Kutolea huduma ya kusafisha mimba zilizoharibika Kwa akina mama wajawazito (Comprehensive Post Abortion Care)
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.