Benki ya CRDB kanda ya kusini imetoa msaada wa vifaa tiba katika kituo cha Afya Likombe Pamoja na msaaada wa chakula na vifaa katika kituo cha makao ya Watoto wenye ulemavu cha Upendo Rehabilitation Day Care Center ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani,
Akikabishi msaada huo, Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali wa Benki hiyo, Bi. Veronica Muumba ametaja msaada uliotolewa katika kituo cha Afya Likombe kuwa na Pamoja na vifaa vya kujifungulia (Delivery kits) 100, Dawa za usafi 50, Chandarua 30, Barakoa PC 200, Reki 10, kwanja 10, fagio 40 na Ndoo maalum ya kudekia.
Na kw kituo cha upendo msaada uliotolewa umejumuisha unga, mchele, mafuta ya kupikia,taulo za kike, juisi, dawa za meno,maji, mafuta ya kupaka, sabuni ya unga, na changamoto.
Amesema kwakua huu ni mwezi wa maadhimisho ya siku ya wanawake, kama taasisi wameona ni vyema kuwashika mkono wanawake ili waepukane na changamoto za kujifungua, ikiwa ni sehemu yao kurudisha kwa jamii.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara – Mikindani, Mhe. Shadida Ndile ameipongeza Benki hiyo kwa kuunga jitihada za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwasaidia wanawake kwenye uzazi salama na kuwataka wadau wengine kuiga mfano huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo cha Upendo, Bi. Christina Chacha mbali na kushukuru kwa msaada huo, ameiomba Serikali na wadau wengine kumsaidia kupata wataalamu wa mazoezi tiba ili kituo hicho kitoe huduma stahiki kwa Watoto wenye usonji kituoni hapo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.