---DAMPO LA KISASA MANGAMBA KUANZA KUTUMIKA HIVI KARIBUN
Kufuatia ziara ya siku mbili ya ukaguzi wa miradi inayotekelezwa na Benki ya Dunia kupitia Mradi wa Uendelezaji wa Miji Mkakati(TSCP) imeshauriwa dampo
la kisasa Mangamba lianze kutumika kwa kuwa asilimia 100 ya ujenzi wa dampo hilo umekamilika. Ushauri umetolewa kwenye kikao cha pamoja cha tathmini ya ziara
kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa Mtwara-Mikindani siku ya tarehe 4 April 2017 ambapo kiongozi wa timu hiyoMhandisi Ezron Kilamhama alimshauri
Mkurugenzi kufungua dampo hilo haraka Pamoja na ushauri huo timu ya ukaguzi pia ilimtaka Mkurugenzi kufanyaMatengenezo ya mara kwa mara kwa miundombinu
ambayo imeshajengwa kama barabara ilikufanya mradi kuwa endelevu Nae Mkurugenzi wa Manispaa Mtwara-Mikindani Beatrice Dominic aliishukuru benki ya Dunia kwa
kuendelea kuisadia Manispaa, lakini pia aliishukuru TAMISEMI kwa kusimamia mradi na kutoa ushauri wa mara kwa mara kwenye uendeshaji wa mradi huo. Aidha aliahidi
kuyafanyia kazi maagizo yote pamoja na ushauri uliotolewa ilikuhakikishamiradi hiyo inakuwa endelevu Ziara hiyo iliyohusu ukaguzi wa uendeleaji wa ujenzi wa Dampo la kisasa lililopo
Mangamba pamoja na ujenzi wa mifereji ya Maji ya Mvua kwa fedha za nyongeza zilizotolewa kwa awamu ya kwanza(AF1), pamoja na ukaguzi wa maeneo na michoro ya awali ya miradi
mingine inayotarajiwa kutekelezwa hivi karibuni kwa fedha za nyongeza za awamu ya pili(AF2),ilianza tarehe 3-4 April 2017 na ilijumuishaWataalamu kutoka TAMISEMI pamoja wawakilishi kutoka
Benki ya Dunia. Mradi wa ujenzi wa dampo la kisasa la Mangamba umetekelezwa katika awamu mbili. Awamu ya kwanza ilianza kutekelezwa Mwezi Machi 2013 na kukamilika Mwezi disemba
2014 na awamu ya pili umeanza Julai 2016 na utaishia Juni 2017. Mpaka Mradi huu kukamilika utagharimu kiasi cha Tsh 7.9bilioni.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.