Ikiwa tupo kwenye wiki ya maadhimisho ya mji mkogwe wa mikindani oktoba 6 mwaka huu,Katibu tawala wa wilaya ya Mtwara Bi. Kasilda Mgeni amewataka wananchi wa mikindani na watanzania kwa ujumla kutembelea mji mkongwe wa Mikindani na kujifunza mambo mbalimbali ya kihistoria.
Amesema kuwa uwepo wa mji huo wa Mikindani ni fursa kwa wakazi wa Mikindani na watanzania kwa ujumla katika kukuza utalii.
Kasilda amezungumza hayo oktoba 2,2018 alipotembelea mji mkongwe wa Mikindani na kujiona sehemu za majengo ya kale kwa ajili ya kupata historia.
Ameongeza kuwa pamoja na Mikindani kuwa mji wa kihistoria lakini pia ni moja ya sehemu ya kukuza uchumi kama wananchi watatembelea maeneo kwa ajili ya kujifunza.
Aidha amewataka wananchi wa mikindani kuhakikisha kuwa wanaimarisha ulinzi na usalama wa miundombinu ya kihistoria iliyopo katika eneo hilo.
“niwasihi wananchi wa mikindani kuhakikisha ulinzi na usalama wa eneo hili linakuwa mikononi mwenu hivyo kila mkazi ana wajibu wa kulinda eneo hili,alisema Kasilda
Mji mkongwe wa Mikindani umetangazwa kuwa mji wa kihistoria katika tangazo lililotolewa katika gazeti la Serikali la tarehe 25 Agost 2018 tangazo namba 308 namba 103. Aidha uzinduzi wa mji huo unafanyika Oktoba 6, 2018 ukiwa na kauli mbiu inayosema “Mikindani lango la utalii kusini,urithi wetu tuutunze na tuuthamini”
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.