Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan amemuagiza MKurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kutoa notisi ya kimaandishi ya kusudio la kufuta umiliki wa hati ya eneo lililopo Mtaa wa Mnazi Mmoja eneo la LItingi linalomilikiwa na Kampuni ya Social Environment and Cultural Communication Ltd Lenye ukubwa wa Ekari 73.
Mkuu wa Wilaya ametoa agizo hilo Julai 6, 2021 alipotembelea eneo hilo lililopo Kata ya Mitengo ( Pembezoni mwa bahari ya Hindi) baada ya kuvamiwa na wananchi waliojenga nyumba za kuishi kutokana na mmiliki wa eneo hilo kutoliendeleza kwa zaidi ya miaka thelathini tangu amemilikishwa licha ya kulipia Kodi ya ardhi kila mwaka.
Sambamba na agizo hilo Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi wenye tabia ya kuvamia meneo na kujimilikisha kiholela kuacha mara moja huku akiwaasa wanasiasa na Viongozi Kutojiingiza kwenye maswala ya uvamizi wa ardhi ili kupunguza migogoro ya ardhi.
'Viongozi tuhakikishe tunasimamia ardhi yetu vizuri, si vema kuona kwenye maswala yahusuyo uvamizi wa ardhi mnahusika moja kwa moja, tushirikikiane katika kuhakikisha wananchi wetu hawajimilikishi ardhi kiholela ili kupunguza malalamiko ya ardhi' amesema Kyobya
Aidha Kyobya ameahidi kukutana na wananchi waliovamia eneo hilo siku ya Ijumaa Julai 9,2021 ili aweze kuzungumza nao na kutafuta suluhu ya jambo hilo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.