Baada ya Zahanati ya Ufukoni kupokea fedha kutoka Serikali kuu kiasi cha Tshs 250,000,000 kwa ajili ya Upanuzi wa Zahanati hiyo kuwa Kituo cha Afya, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya amemuagiza Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi. Tamko Ally kuharakisha mchakato wa ununuzi wa vifaa kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya Zahanati hiyo ili kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.
Amesema kuwa ucheleshwaji wa ununuzi wa vifaa utapelekea ujenzi huo kutokamilika kwa wakati na kusababisha adha kwa wananchi kuendelea kufuata huduma katika maeneo mengine.
Mhe. Kyobya ametoa rai hiyo Novemba 4,2021 katika Ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ilipotembelea kukagua Utekelezaji wa Ujenzi wa Madarasa katika Manispaa yetu.
Aidha amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi na kushiriki kikamilifu katika ujenzi huo ili kuiongezea nguvu Serikali.
“Kama tulivyoshirikiana katika miradi mingine nawaomba tujitokeze kushiriki kimamilifu maana hiki Kituo cha Afya ni cha sisi wananchi”Amesema Kyobya
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi. Tamko Ally amemhakikishia Mhe. Kyobya kuwa mchakato wa un ununuzi wa vifaa vya ujenzi utaharakishwa kama alivyoagiza.
Bi. Salima Namenya Mkazi wa Kata ya Ufukoni amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Mhungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha za upanuzi wa Zahanati ya Ufukoni kuwa Kituo cha Afya kwani Kituo hicho kitapanua wigo katika utoaji wa huduma za Afya.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.