Ikiwa imepita miezi ishirini na mbili tangu Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya alipoahidi kutoa zawadi ya shilingi milioni moja kwa kila mwanafunzi atakaefaulu vizuri kwa daraja la kwanza pointi tatu kidato cha sita na daraja la kwanza pointi saba kwa kidato cha nne kwenye Mitihani ya Taifa Juni 21,2020, Leo Machi 31 ametimiza ahadi yake kwa kukabidhi shilingi milioni mbili kwa wanafunzi wawili wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Mtwara waliofaulu kwa kupata daraja la kwanza pointi saba katika Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha nne uliofanyika mwaka uliopita.
Pamoja na wanafunzi hao Mhe. Kyobya pia ameahidi kukabidhi milioni tano kwa wanafunzi wengine watano kutoka Shule ya Sekondari Mtwara Ufundi (mwanafunzi mmoja) na wanafunzi wanne wa Shule ya Sekondari sabodo ambao pia wamefaulu kwa daraja hilohilo .
Mkuu wa Wilaya amekabidhi zawadi hizo leo Machi 31,2022 kwenye mahafali ya 56 ya wanafunzi wa kidato cha sita kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana Mtwara.
Aidha Mhe.Kyobya amesema kuwa Pamoja na kutoa zawadi kwa wanafunzi hao anajipanga pia kutoa zawadi kwa walimu wote waliofaulisha vizuri kwenye matokeo ya Mtihani huo.
Ameendelea kusisitiza kuwa utoaji wa zawadi na motisha utakuwa endelevu na utakuwa unafanyika kila mwaka ili kuleta hamasa kwa wanafunzi na walimu ili waongeze bidii kwenye kujifunza na ufundishaji.
Amewataka wanafunzi wanaomaliza kwa muda uliobaki wautumie vizuri ili wafaulu vizuri kwani nanahitaji kila mmoja afaulu kwa daraja la kwanza pointi tatukatika kuhakikisha wanawanafunzi wengine na walimu ili
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.