Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya amewataka walimu wakuu, wakuu wa shule na watendaji wa Kata Manispaa ya Mtwara-Mikindani kuwashirikisha wadau wa maendeleo ili waweze kuchangia utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Maendeleo katika sekta ya elimu.
Kyobya ametoa rai hiyo leo Machi 5,2021 alipofanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu ya shule na masuala mbalimbali ya maendelo katika shule za Msingi na Sekondari zilizopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Amesema kuwa Pamoja na Serikali kufanya mambo mengi katika sekta hiyo bado ushiriki wa wananchi ni muhimu katika kujitolea ujenzi na kuchangia vitu mbalimbali ili kuweza kusukuma gurudumu la maendeleo.
Wakati huohuo Kyobya pia amempongeza Mkurugenzi wa manispaa hiyo Col. Emanuel Mwaigobeko kwa kazi kubwa anayoifanya ya kutoa fedha kutoka mapato ya ndani na kujenga madarasa Pamoja na utengenezaji wa madawati, viti na meza.
Aidha amewasisitiza wakuu wa shule na walimu wakuu kuendelea kupanda miti ya matunda katika maeneo ya shule zao ili waweze kunufaika na vivuli Pamoja na matunda.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya Pamoja na timu aliyoambatana nayo wameahidi kuchnagia madawati thelathini na mbili yatakayosaidia kupunguza changamoto ya madawati iliyopo ndani ya Mnaispaa
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.