DC MMANDA AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI MANISPAA MTWARA-MIKINDANI.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evod Mmanda tarehe 30 Oktoba 2017 amefanya ziara ya Ukaguzi wa Miradi mbalimbal ya Maendeleo inayotekelezwa na halmashauri ya Manispaa-Mtwara Mikindani.
Ziara hiyo ilikuwa na lengo na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Miradi lakini pia kukagua nakuona maghala ya korosho kwa kuwa msimu umeshaanza.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na mradi wa ujenzi wa miundombinu ya afya katika Zahanati ya Likombe inayohusisha ujenzi wa wodi ya mama na watoto, Ujenzi wa Nyumba ya Mtumishi, Ujenzi wa maabara, Ujenzi wa kichomea taka, ujenzi wa sehemu ya kufulia pamoja na ujenzi wa chumba cha kuhifadhi maiti.Katika mradi huo mkuu wa wilaya amenesha kuridhika na kasi ya ujenzi unaoendelea.
Pia Mkuu wa Wilaya alikagua mradi mwingine wa Ujenzi wa Zahanati ya Mbawala Chini iliyojengwa kwa nguvu ya wananchi kwa kushirikiana na Halmashauri. Mradi huu uliibuliwa na Wananchi wenyewe na wametoa hekari tano Kwa ajili ya ujenzi na kufyatua tofali 4000. Aidha halmashauri kwenye bajeti yake ya 2017/2018 imetenga shilingi milioni 40 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati hiyo na tayarai milioni 10 zzimepelekwa kwenye Kata ili mradi uanze kutumika
Pamoja na mirdai hiyo pia alitembelea kwenye maghala ya korosho yaliyopo mikindani na Naliendele na kujiona suala zima la utunzaji wa korosho utekelezaji wa mfumo wa stakabadhi ghalani. Aidha kwenye maghala ya korosho imebainika kuwa wakulima wengi wanachukua korosho aina ya tegu na kuzifungia kwenye gunia kwa ajili ya kupima.
Hivy Mkuu wa Wilaya amewataka vyama vya msingi kuhakikisha ubora wa korosho kabla ya kuzipima kwa maana mkulima anapopeleka korosho kwa ajili ya kuzipima zinamwaga chini ili ziweze kkaguliwa halafu baada ya hapo zipimwe ili mulima na mnunuzi kla mtu apate anachostahili
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.