Mkuu wa wilaya ya Mtwara Mhe. Hanafi Msabaha amezitaka taasisi zisizo za kiserikali kuzingatia taratibu, sheria na kanuni za uendeshaji wa taasi hizo na kufuata sheria za nchi katika kuendesha taasisi ili kuleta maendeleo katika jamii husika.
Amezisisitiza taasisi hizo kutimiza vigezo vyote ikiwemo usajili ili kuweza kutambulika na Serikali kulingana na shughuli zitakazofanyika kwenye taasisi hizo.
Amesema kuwa kwa sasa wananchi wa Mtwara wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo changamoto ya mmomonyoko wa maadili akitolea mfano wa kulipotiwa kwa kesi nyingi za ubakaji na ulawiti vilevile changamoto ya kupolomoka kwa uchumi,hivyo amezitaka taasisi hizo kuwajengea uwezo wananchi kwa kuwaonyesha fursa za kiuchumi na kuibadili jamii katika kulinda maadili na mira na desturi za jamii zetu.
Msabaha ameyasema hay oleo Mei 26,2023 kwenye mkutano wa Wilaya wa Taasisi zisizo za kiserikali zilizomo katika Wilaya ya Mtwara kilichofanyika katika ukumbi wa Manispa ya Mtwara-Mikindani chenye lengo la kufahamu mchango wa taasisi zisizo za kiserikali katika kuleta maendeleo.
Aidha wamewataka kufanya kazi kwa kushirikiana na Serikali kwa kuzingatia miongozo na malengo ya serikali ili kuepuka tasisi kufanya kazi zinazofanana.
Hata hivyo Msabaha alisema kuwa seriali itaendelea kufatilia na kuzifutia usajili taasisi zenye lengo la kuharibu mira na tamaduni za jamii zetu,hivyo amezisisitiza tasisi hizo kutokubali matakwa ya kiuchumi kutoka katika nchi za nje.
Nae Mkurugenzi wa Manispaa Mtwara-mikindani COL.Emanuel Mwaigobeko amesema kuwa Taasisi hizo zisizo za kiserikali zilizopo Manispaa ya Mtwara Mikindani zimesaidia kubaini na kutatua changamoto mbalimbali zinazowahusu wananchi kwa ujumla.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.