Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya ameagia kutolewa kwa elimu ya masuala ya lishe sambamba na uhamasishaji kwa wananchi wa Kata 18 kulima mboga mboga majumbani ili kuongeza hamasa kwa wananchi ya kula mlo kamili.
"Leo tumeshuhudia uingiaji wa mikataba ya lishe kati ya Mkurugenzi na Maafisa watendaji wa Kata 18 , Afisa utumishi na Maafisa watendaji wa Kata
'Niombe Elimu ya lishe ifike kwa watu wote , vikundi vyote na shuleni ili tupate uelewa , zianzishwe bustani ndogondogo kwa kila kaya na wahakikishe suala la lishe linaeleweka vizuri kwa watu wote na waweke utaratibu wa kuweka orodha ya chakula na picha zake ili kila kaya jambo la lishe liwe ni ajenda"
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani COL. Emanuel Mwaigobeko amesema kuwa kikao hicho cha afua za lishe ngazi za Kata hufanya tathmini ya utekelezaji wa afua za lishe kwa robo ya kwanza.
"Utekelezaji ulikuwa mzuri mwaka jana tulikuwa watatu Kitaifa na tumekuwa tukiboresha kila mwaka, natoa wito kwa wananchi kuzingataia lishe wengi wanakula bila kujali chakula wananchokula kinawasaidia nini"
"unatakiwa kila unapokula ujue kinakusaidia nini ipo haja ya kla vyakula tofauti ili kuboresha afya yako
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.