Baada ya ugeni kutoka Mji wa PforzheimUjerumani kutembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Julai 14,2022 Mhe. Dunstan Kyobya amewataka wageni hao kutembelea Mji Mkongwe wa Mikindani na vivutio vingine vya utalii na kuwakaribisha kuja kuwekeza Mtwara kwa kuwa Mji huu unafikika kwa urahisi na una vivutio vingi ikiwemo fukwe nzuri.
Aidha amewaomba wageni hao kuwa mabalozi wazuri wa kuitangaza Mtwara wakirudi Ujerumani na amewasisitiza kuendeleza na kuimarisha urafiki uliopo baina yao na Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.