Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evod Mmanda Julai amewataka Maafisa Elimu wa Kata Manispaa ya Mtwara-Mikindani kutozigeuza bodaboda pikipiki walizogawiwa na Serikali badala yake pikipiki hizo zikatumike kwa kazi zilizokusudiwa.
Mmanda amezungummza hayo julai 17,2018 kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya pikipiki 18 kwa waratibu elimu wa Kata 18 za Manispaa ya Mtwara-Mikindani, hafla hiyo ilifanyika kwenye kwenye viwanja vya Ofisi ya kuu ya Manispaa.
Amesema kuwa Serikali imefanya jambo kumbwa sana katika kurahisisha utendaji kazi wa waratibu hao kwa kuwawezesha pikipiki zitakazowasaidia kutembelea shule walizokuwa nazo na kuhamasisha shughuli mbalimbali za elimu kwenye maeneo yao ili kuleta matokeo hanya.
“kwa sas hamtakuwa na sababu ya kushindwa kufanya ukaguzi kwenye shule zenu kwa kuwa munao usafiri hivyo ninatarajia kuona kiwango cha ufaululu kinaongezeka “alisema Mmanda
Aidha amewasiistiza waratibu hao kuzitunza pikipiki na kuzitumia kwa kazi zilizokusudiwa kwani kufanya hivyo pikipiki hizo ztadumu kwa muda mrefu.
“hizi pikipiki ni za serikali ni lazima muzitunze, tusije tukazikuta zinageuzwa kuwa bodaboda, tusije tukazikuta sehemu zisitakiwa na kwa muda usiotakiwa, mali ya serikali kama tunavyofahamu zina utaratibu wake”alisistiza mmanda
Pamoja na zoezi hilo pia Mmanda amewataka waratibu kusimamia na kufafanua waraka unaohusu wazazi na walezi kuwajibika kwenye uchangiaji wa upatikanaji wa chakula cha mchana shuleni ili wanafunzi waweze kusoma vizuri.
Akizungumza kwa niaba ya waratibu wenzake Mwalimu Florence Magomba ameishukuru Serikali kwa kuwawezesha pikipiki hizo zitakazosaidia kutembelea shule na kuahidi kufanya kazi ya ziada zitakazopelekea kuboresha elimu na kupandisha ufaulu.
Zoezi la ugawaji wa pikipiki kwa waratibu Elimu wa Kata limezinduliwa Julai 4 jijini Dar es salaam na Waziri…………… aidha jumla ya pikipiki 2894 zitagawiwa kwa waratibu elimu wa Kata nchini.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.