Kutokana na kuwepo kwa changamoto mbalimbali katika sekta ya afya Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mkuu wa wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya amewataka wadau mbalimbali wa maendeleo kuchangia katika sekta hiyo ili kuweza kutatua changamoto zilizopo.
Kyobya ametoa wito huo Mei 20,2020 wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa bodi mpya ya afya ya Manispaa ya Mtwara-mikindani iliyoteuliwa Novemba 1 mwaka jana .
Amesema kuwa kwa upande wa Serikali imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kuimarisha sekta ya afya kwa kujenga vituo vya afya na usambazaji wa vifaa tiba hivyo wadau wa maendeleo wakiunga mkono jitihada hizi za Serikali Manispaa itasonga mbele.
Aidha Kyobya amewapongeza wajumbe wapya wa bodi walioteuliwa na kuwataka kufanya kazi kwa kuzingantia taratibu, miongozo na kanuni ili kuweza kushauri vizuri kamati za afya zilizopo kwenye Zahanati .
“Afya ndio jukumu la msingi, mna kazi kubwa ya kusimamia na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kutatua changamoto zilizopo katika sekta ya afya”alisema Kyobya.
Kwa upande wake Kaimu MKurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bwana Grayson Orcado amesema kuwa ana imani na wajumbe wa bodi walioteuliwa kuwa watafanya kazi kwa namna ambayo itasaidia na kuboresha afya za watanzania hasa wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani na hata wananchi wanaotokea katika halmashuari zingine.
Awali akisoma taarifa ya afya Mganga Mkuu wa Manispaa Dkt. Joseph Kisala amesema kuwa bodi iliyoteuliwa na kuzinduliwa ni bodi ya pili na itadumu kwa muda wa miaka mitatu ,aidha bodi hiyo itasimamia Vituo ishirini na mbili vikiwemo Vituo vya afya vinne na zahanati kumi na nane.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.