Kuelekea kwenye Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Mwanahamisi Munkunda ameungana na wananchi na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali kwenye maombi ya Dua ya kuwaombea viongozi pamoja na kuliombea Taifa letu la Tanzania.
Akizungumza mara baada ya Dua leo April 22,2024 iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Munkunda amewapongeza viongozi wa dini kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwaombea wananchi, viongozi na Taifa kwa ujumla na kuwafanya wananchi wa Tanzania kuwa familia moja yenye upendo amani na utulivu.
Amesema kuwa zipo nchi zinazojaribu kuvuruga familia ya Tanzania lakini kutokana na uimara wa viongozi waliopo ngazi za juu ambao wamelelewa katika misingi ya Dini pamoja na mila na desturi za watanzania ya kuwa na umoja muda wote na ndio maana Tanzania imekuwa Salama hadi sasa.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bi.Bahati Geuzye amesema maadhimisho ya miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yataambatana na Shughuli mbalimbali katika kila Wilaya zikiwemo Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo pamoja na mikesha katika wilaya zote za Mkoa wa Mtwara huku akiwataka viongozi kuhamasisha wananchi kujitokeza kushiriki kuliombea Taifa na kuwaombea viongozi kwenye mikesha a dua kwenye kila Wilaya.
Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano mwaka yanakwenda na Kauli mbiu inayosema “Tanzania Tumeshikamana na Tumeimarika,kwa Maendeleo ya Taifa Letu.”
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.