Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe.Mwanahamisi Munkunda ameunda kamati ya watu kumi na moja inayowahusisha wafanyabiashara wa Stendi ya Mkanaredi na watumishi kutoka kwenye ofisi yake watakaofanya kazi kwa siku saba kuanzia Agosti 12,2024 kwa ajili ya kushughulikia malalamiko mbalimbali yaliyotolewa na wafanyabaishara hao ili aweze kufanya maamuzi kutokana na mapendelezo yatakayotolewa na kamati hiyo.
Akizungumza mara baada ya kuunda Kamati hiyo Agosti 5,2024 ,Mkuu wa Wilaya ameitaka Kamati kufanya kazi kwa uaminifu ili iweze kuleta mapendekezo yatakayokuwa na suluhisho la kudumu kwa changamoto zilizotolewa.
Aidha amewataka wataalamu wa Manispaa ya Mtwara -Mikindani wanapotaka kufanya mabadiliko yoyote katika eneo hilo wakae pamoja na wafanyabiashara ili kuondoa manung’uniko na kero kwa wananchi.
Nae Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mwalimu Hassan Nyange ameahidi kutatua changamoto zilizobainishwa na wafanyabiashara hao ikiwemo ukarabati wa choo, kuweka Taa nyakati za usiku pamoja na kutuama kwa maji katika stendi hiyo wakati wamsimu wa mvua.
Akizungumzia suala la ujenzi wa Stendi mpya ya kisasa Mwalimu nyange amesema kuwa tayari ofisi yake imekamilisha taratibu zote na muda si mrefu Ujenzi utaanza na kuongeza kuwa stendi inayotumika sasa itafanyiwa ukarabati kwa kuweka zege nzito kwa ajili ya magari ya mizigo (malori).
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.