Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe, Abdallah Mwaipaya amewataka wanawake wa Wilaya hiyo kuitumia siku ya wanawake duniani kutafakari changamoto mbalimbali zinazowakabili, kuzipatia majibu na ufumbuzi wa kudumu.
DC Mwaipaya ameyasema hayo jioni ya Machi 07, 2025 katia iftari maalum iliyoandaliwa na wanawake wa kata ya Mtonya wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Mhe. Shadida Ndile na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali.
Alisema kwasasa dunia imebadilika na kwa kiwango kikubwa maendeleo yamebebwa na wanawake, hivyo ni vyema wakaendelea kuchangamkia fursa mbalimbali zinazijitokeza.
Aliongeza kwa kutoa wito kwa wanawake hao kutumia kipindi hiki cha mfungo kuliombea Taifa linapoelekea kwenye uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Aidha, amewasisitiza wanawake katika jamii kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Dtk. Samia Suluhu Hassan katika kuwaunganisha watu na kuwa wamoja.
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, Mhe, Shadida Ndile amesema kuwa maandalizi ya Iftari hivyo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyoambatana na ufanyaji wa shughuli mbalimbali za kijamii.
Kwa upande wa kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, Gwasika Mwasyeba, alitumia fursa hiyo kutoa rai kwa wafanyabiashara kutopandisha bei za mahitaji mbalimbali ikiwemo vyakula katika msimu huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na Kwaresma ili wananchi wafurahie funga yao.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.