Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe. Abdalah Mwaipaya, amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa Mtwara-Mikindani, Mwalimu Hassan Nyange kwa usamimizi imara wa Miradi ya Maendeleo na kufanikisha kukamilika kwa wakati na Ubora unaotakiwa.
Ameyasema hayo Leo Oktoba 03, 2024 wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa Zahanati ya Magomeni pamoja na mradi wa Ujenzi wa shule ya mpya ya Sekondari yaTandika.
Amesema pasi na shaka Halmashauri ya Mtwara Mikindani ni mfano wa kuigwa katika usimamiizi wa Miradi ya Maendeleo.
"Nakupongeza sana Mkurugenzi kwa maamuzi yako na usimamizi wenye matokeo chanya, nawapongeza sana na niwatie moyo, Mnafanya kazi nzuri!," amesema Mhe. Mwaipaya.
Sambamba na hilo Mhe. Mwaipaya amewapongeza wananchi wa kata ya Tandika kwa kushiriki ujenzi huo, kwani nguvu zao zimepelekea kupunguza gharama za Ujenzi wa mradi huo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Nyange amesema, Mradi wa Ujenzi wa Shule ya Sekondari Tandika unatarajiwa kuweka jiwe la msingi na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Stergomena Tax Oktoba 6,2024, na Ujenzi unatarajiwa kukamilika rasmi tarehe 30 mwezi huu.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.