Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe. Abdalah Mwaipaya amewasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili watumie haki yao ya kidemokrasia kupata viongozi sahihi wataongoza vyema Mitaa yao.
DC Mwaipaya ametoa rai hiyo 25 Novemba 2024 wakati wa kuhitimisha michuano ya 'Uchaguzi Ndile Cup' iliyofanyika katika uwanja wa shule ya Msingi Chikongola, Kata ya Tandika, na kushuhudia timu ya kata ya Mtonya ikiibuka bingwa wa michuano hiyo.
Alisema muda mchache umebaki kufikia siku ya Jumatano 27 Novemba 2024, ambayo ndiyo siku rasmi ya Kitaifa kwa wananchi wote waliojiandikisha kupiga kura kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa hivyo ni vema Kila Mwananchi aliyejiandikisha kupiga kura.
Aidha, alitumia hadhara hiyo kumpongeza Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, Mhe Shadida Ndile, kwa kuanzisha Michuano hiyo iliyowakutanisha wananchi kwa wingi na kupata elimu na hamasa kuelekea Uchaguzi huo.
Bingwa wa Michuano hiyo Kata ya Mtonya alijitwalia Kombe na fedha taslimu Shilingi Milioni Moja, wakati Mshindi wa pili (Kata ya Jangwani) akijinyakulia fedha taslimu Shilingi Laki Tano.
Katika Mchezo huo wa fainali pia ilishuhudiwa na Mkurugenzi wa Manispaa Mtwara-Mikindani, Mwalimu Hassan Nyange, Katibu Tawala wa Wilaya (DAS), Mwinyi Ahmed Mwinyi pamoja na viongozi wengine wa Chama na Serikali.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.