Mkuu wa Wilaya yAa Mtwara Abdallah Mwaipaya amewaasa waandihsi wa habariwilayani hapa kuitendea haki taaluma yao kwa kufuata misingi ya uandishi katika kuhabarisha kuelekea zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Amesema waandishi wa habari ni nyenzo muhimu sana katika kutoa elimu na kuhamasisha wapiga kura hivyo ni vema kutumia weledi katika kuhabarisha ili kutimiza malengo tarajiwa ya zoezi hilo.
DC Mwaipaya ameyasema hayo leo alipokutana na waandishi wa habari toka vyombo mbalimbali vya habari wilayani Mtwara ili kuzungumzia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu.
"Hakikisheni mnalinda taaluma, maadili ikiwa ni pamoja na kufuata misingi ya uandishi Kwa kuandaa habari zenye tija kuelekea zoezi hili," alisema.
Aliongeza kuwa ni muhimu waandishi wa habari kuandaa vipindi vya maoni 'Vox pops' kwaajili ya kupata maoni ya wananchi ili kuwahamasisha kujiandikisha, kupiga kura pamoja na kugombea nafasi mbalimbali.
Sambamba na hilo amewasihi Viongozi wenzake kuwatumia vyema waandishi wa habari kutangaza Maendeleo yanayofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.
"Huwezi kufanikisha agenda yeyote bila kushirikisha vyombo vya habari, ..'information is power',"
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.