Zaidi ya vijana 250 wa Tarafa ya Mikindani Leo Oktoba 19,2024 wamefanya matembezi yaliyoandaliwa na Diwani wa Kata ya Mtonya Mhe. Shadida Ndile ambayo yalilenga kuhamasisha vijana ambao bado hawajajiandikisha ili wajitokeze kujiandikisha kwenye daftari la orodha ya wapiga Kura na kujitokeza kupiga kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27,2024.
Akizungumza mara baada ya Matemebzi hayo Mhe. Ndile amewataka vijana hao kupita nyumba kwa nyumba kwa siku moja iliyobaki ili kuhamasisha ndugu, jamaa na marafiki ambao bado hawajajiandikisha waende wakajiandikishe ili waweze kuwa wapiga kura halali.
Amesema kuwa pamoja na kuwapa vijana hamasa ya Uchaguzi lakini matembezi hayo pia yamelenga kuwajenga vijana kuwa na uzalendo na nchi yao pamoja na kuwakutanisha na viongozi wa juu akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara COL. Patrick Sawala ili aweze kuzungumza nao juu ya masuala mbalimbali yanayohusu nchi yao.
Matembezi hayo yalianzia Stendi ya mabasi ya Mikindani na Kuishia Chuo Cha Uvuvi Cha FETA kilichopo Mtaa wa Mirumba Kata ya Jangwani ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara alizungumza nao.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.