Kampuni ya Habari ya IPP MEDIA kupitia kituo chake cha habari cha East African Radio/ Television imegawa makasha alfu moja mia nane ishirini na nne ya taulo za kike kwa wanafunzi wasichana wa shule nne za Sekondari nne ….. kupitia Kampeni yake ya Namthamini nasimama naye iliyolenga kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wasichana na kupunguza uwezekano wa kupata mimba za utotoni.
Bi.Najma Paul mtangazaji kutoka East Africa Radi/Televison amesema kuwa Kmapeni ya Namtah,ini nasimama nae inatoa taulo za kike kwa Watoto ili kumuwezesha aweze kusoma vizuri darasani na kufaulu na kufanikiwa kenye masomo yao.
Amesema kuwa Kampeni hii pia inatoa elimu ya wanafunzi wa kike kujitambua na kutambua haki zao za Msingi lakini pia inawataka kuwa majasiri wa kueleza changamototo wanazokumbana nazo kwenye jamii ili waweze kusaidiwa kabla hawajapata madhara.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe.Dunstan Kyobyaamempongeza Mstahiki Meya wa Mnaispaa ya Mtwara-Mikindani Shadida Ndilekwa kuwatafuta wadau hao na kuja kuwasaidia wanafunzi wa kike.
Aidha ameashukuru East Afrix redio /Televuson kwa kutoa taulo za kike na amewataka wananfunzi wa wavulana kuacha tabia ya kuwacheka wanafunzi wa kike pale wanapopatwa na na changamotoya hedhi badala yake wawasaidia kwa kuwahifadhi,kuwastiri na kuwaheshimu.
Kwa upande Mstahki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi.Shadida ndile amewapongeza wadau hao kwa kuwajali watoto m wa kike huku akiwaasa wanafunzi wa kike kutumia muda mwingi kwenye kujifunza.
Akiongea kwa niaba ya wanafunzi wenzake Ashura DSelemani mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Naliednele ameishukuru East Africa Radio kwa kuwawezesha taulo za kike na ameahidi kusoma kwa bidii ili waweze kufikia malengo yao.
Wanafunzi walipatiwa taulo za kike wanatoka katika Shule za Sekondari za Mikindani, Naliendele na Mangamba.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.