Ikiwa zimepita Siku 9 tangu ufunguzi wa tamasha la Mtonya (FESTIVAL FESTIVAL) lifunguliwe Septemba, Leo Septemba 2,,2024 ni Siku ya fainali ya tamasha hilo ambalo limeanza Kwa kishindo asubuhi Kwa kufajyika Kwa mbio za pole pole (jogging) na ufanyaji wa usafi wa Mazingira kuzunguka Eneo la stendi ya Mikindani.
Diwani wa Kata ya Mtonya (Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani) ameongoza matukio hayo akiwa sambamba na Naibu Meya wa Meya Mhe. Sixmund Lungu pamoja na diwani viti maalumu (mlezi wa Kata ya Mtonya) Mhe. Mwanahamisi Libuburu.
Mstahiki Meya amewashukuru wadau wote waliohudhuria matukio hayo na amewasisitiza kuendelea Kufanya mazoezi ili kujikjnga na magonjwa mbilimbili pamoja na kuzingatia Usafi wa Mazingira katika Maeneo hayo.
Mstahiki Meya ametumia matukio hayo kuwahamasisha wanawake na Vijana Kushiriki kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Fainali za Mtonya Festival litafanyika jioni ya Leo katika Kata ya Mtonya huku Mgeni rasmi akutarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe.Abdallah Mwaipaya
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.