‘’FANYENI KAZI BILA UPENDELEO’’AMOUR A. AMOUR"
Watumishi Wa Serikali wametakiwa kufanya kazi za kuwatumikia wananchi kwa usawa bila ya kujali itikadi za vyama, dini,rangi au makabila.
Aidha amesema kuwa wakati wanakimbiza mwenge wa uhuru anakagua mradi wa kiwanda cha korosho amekuta wafanyakazi wengi ana imani ndani ya kiwanda hiko hata wazanzibar wapo hivyo
Hayo yamesemwa na kiongozi wa mbio wa mbio za mwenge wa uhuru 2017 Ndugu Amour A.Amour mnamo tarehe 20/5/2017 wakati anahutubia wananchi katika viwanja vya mashujaa Vilivyopo Manispaa ya mtwara-Mikindani.
Amour amesema kuwa viwanda vinavyofufuliwa vinaongeza ajira kwa wananchi hasa vijana na kuinua hali ya uchumi ya wananchi wa Mtwara na Tanzania kwa ujumla kwa usawa bila kujali itukadi yoyote.
Aidha Amour ameipongeza Manispaa kwa kutenga aslimia tano ya fedha za mapato yake ya ndani katika kutoa mikopo kwa Wanawake na Vijana na kuwataka Maafisa Maendeleo ya Jamii kusimamia vikundi hivyo na kutoa elimu ya kutosha ili waweze kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.
Pia ameipongeza Manispaa ya mtwara mikindani kwa kuwa na mradi mkubwa wa kudhibiti wa taka ngumu kwani uwepo wa mradi huo utasaidia kujikinga na magonjwa mbalimbali kama vile malaria. Lakini pia uwepo wa mradi huo utasaidia kutengeneza ajira kwa vikundi vinavyozoa taka kutoka kwenye kaya na kupeleka dampo.
Mwenge wa Uhuru 2017 umezindua mradi 1, Umeweka jiwe la msingi miradi 3 na imekagua na kuona miradi 4 hivyo kufanya jumla ya miradi 8 imepitiwa na mwenge huo yenye jumla ya kiasi cah Tsh. 10,828,431,626/=.
Aidha katika miradi hiyo Wananchi wamechangia 33,000,000/= sawa na 0.3% , Halmashauri imechangia 243,014,640/= sawa na 2.2%, mchango wa Serikali kuu ni Tsh.3,303,498,922 sawa na 30.5 44.8%, michango kutoka wahisani ni Tsh.4,848,918,064 sawa na 44.8% na michango ya sekta binafsi ni Tsh. 2,400,000,000/= sawa na 22.2%.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.