Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani COL. Emanuel Mwaigobeko amewataka wataalamu wakiwemo Mganga Mkuu, Mhandisi na Afisa Ugavi kusimamia ujenzi wa hospitali ya Wilaya Mjimwema kwa kuhakikisha mafundi wanafanya kazi usiku na mchana ili ujenzi huo uweze kukamilika ifikapo Juni 30 mwaka huu.
Mkurugenzi amesema kuwa ili kutekeleza agizo hilo, Ofisi imeshakamilisha malipo ya awali ya mkandarasi pamoja na ununuzi wa malighafi/ vifaa mbalimbali vya ujenzi vikiwemo matofali, mchanga, saruji na vipo eneo la mradi.
Ikumbukwe kuwa Desemba 2022, Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani ilipokea fedha Shilingi milioni mia tano (500,000,000) kutoka Serikali kuu za awamu ya kwanza kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Mjimwema kwa majengo ya maabara, jengo la kusubiria wagonjwa wa nje (OPD) na ujenzi wa kichomea taka.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.