Shirika Lisilo la Kiserikali la Faidika wote Pamoja (FAWOPA) linalofanya kazi zake Mkoani Mtwara leo Agosti 19 2021 limegawa vifaa mbalimbali vya shule kwa wanafunzi 67 wanaoishi kwenye mazingira magumu kutoka katika shule kumi za Sekondari zilizopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Pamoja na vifaa hivyo FAWOPA pia wamekabidhi fedha taslimu shilingi 418,000 kwa wanafunzi 11 wanaosoma Chuo Cha Maendeleo ya wananchi Mtawanya.
Mkurugenzi wa FAWOPA Batazari Komba amesema kuwa Shirika limekabidhi vifaa hivyo ili kuimarisha Ustawi wa Elimu kwa watoto hao.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.