Baada ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani kupokea shilingi bilioni moja milioni mia tatu kumi na tisa laki moja arobaini mia tano na nane (1,319,140,508) kutoka Serikali kuu kwa ajili ya kutekeleza miradi ya Maendeleo katika robo ya kwanza mwaka 2022 /2023 , Wajumbe wa baraza la Madiwani Manispaa ya Mtwara-Mikindani wamemshukuru na wamempongeza Rais wa Jamhuri.ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Serikali yake kwa kutuletea fedha hizo kwenye sekta mbalimbali zikiwemo elimu, afya na TASAF.
“Jitihada za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali yake tunaiona, Ukizunguka ndani ya Manispaa yetu kila kona miradi inatekelezwa, ni kazi yake na Chama Cha Mapinduzi , Nichukue nafasi hii kwa niaba ya madiwani wenzangu kumshukuru na kumpongeza sana Rais Samia kwa kutuletea fedha za miradi ya Maendeleo” amesema Mhe. Naibu Meya Edward Kapwapwa
Aidha Madiwani hao wamempongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani COL. Emanuel Mwaigobeko kwa kutoa fedha za mapato ya ndani shilingi milioni mia mbili sitini na tisa laki nane themanini na tatu mia tisa ishirini na sita (269,883,926) katika robo hii ya kwanza na kuzipeleka Kwenye Kata kwa ajili ya Utekekelezaji wa Miradi ya Maendeleo
Kwa upande mwingine Madiwani hao pia wamempongeza Mhe. Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Hassan Mtenga kwa kuwezesha vifaa vya ujenzi kwenye baadhi ya Kata zilizopo ndani ya Manispaa.
Wajumbe wa baraza la Madiwani wametoa pongezi hizo Oktoba 27,2022 kwenye mkutano wa baraza la madiwani wa kupitia na kujadili taarifa za Kata uliofanyika kwenye Ukumbi wa shule ya Sekondari ya Mtwara Ufundi.
Miradi inayotekelezwa kwa kutumia fedha hizo ni pamoja na ujenzi wa vyumba ishirini na moja vya madarasa ya Sekondari ( 240,000,000), ujenzi wa nyumba ya mtumishi Mitengo Sekondari mbili kwa moja (114,683,972), Fedha za TASAF (321,740,356), Elimu bure Msingi na Sekondari
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.