Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mikindani Ndugu Gwakisa Mwasyeba akiambatana na Afisa Tarafa ya Mtwara Mjini Tito Cholobi na Mratibu wa Maafa Matwiko Leo Februari 9,2025 wamegawa Unga wa sembe Kg 1825 Kwa baadhi ya wananchi walioathirika na mvua kubwa zilizonyesha Kwa siku tano Kuanzia Februari 3-7,2025 na kusababisha mafuriko yaliyoathiri Nyumba za watu na miundombinu mbalimbali.
Gwakisa amesema Kuwa zoezi lililofanyika Leo ni hatua za awali na kwamba Serikali Mkoani Mtwara itakaa na wadau mbalimbali Kwa ajili ya kuona namna watakavyoshirikiana katika kuwasaidia wahanga wa mafuriko hayo.
Unga huo umepelekwa katika Ofisi za Kata ya Shangani, Rahaleo, Chuno pamoja na Mtonya
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.