Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Hanafi msabaha amesema kuwa ili Wilaya ya Mtwara iweze kufanya mambo mazuri inahitaji ushirikiano baina ya viongozi na wananchi wa Wilaya hiyo huku akiahidi kutofanya jambo lolote peke yake bila ya kuwashirikisha watu hao.
“Hakuna jipya kazi ni ile ile inaendelea, nitaendelea pale pale alipoishia Mkuu wa Wilaya aliyepita, waswahili wanasema tukiupiga mwingi sisi Mama Samia anakuwa ameupiga mwingi na mwaka 2024/ 2025 Mwenyekiti hapa nae atakuwa ameupiga mwingi, tukishirikiana kila kitu kitaenda sawa” amesisitiza Mhe. Msabaha
Aidha Mhe. Msabaha ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha na kuwataka viongozi kutoa taarifa mapema kwenye kila jambo ambalo lina mkanganyiko ili liweze kurekebishwa mapema kabla halijaharibika.
Mhe. Msabaha ameyasema hayo Februari 9,2023 alipokuwa anapokea Ofisi kutoka kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara ambaye sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Dunstan Kyobya.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.