Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mtwara Mjini Mhe. Salumu Naida ameipongeza Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuwahudumia wananchi na usimamizi madhubuti wa miradi ya maendeleo kulikopelekea kuitekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kiwango kikubwa.
Mhe. Naida ameyasema hayo Leo Januari 12,2024 kwenye kikao cha halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Mtwara Mjini kwa ajili ya kupokea utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho ya mwaka mmoja wa 2023-2024 iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe. Abdallah Mwaipaya, katika Ukumbi wa Chuo Cha Ualimu-Masandube.
“Mstahiki Meya nikupongeze kwa kazi kubwa mnayoifanya wewe pamoja na madiwani wako na watumishi wa Manispaa hii, sisi kama Chama Tawala hakika mnatupa matumaini ya kutembea kifua mbele kwa sababu Ilani yetu inatekelezwa vizuri” amesema Mhe Naida
Aidha, Mhe. Naida amewataka wajumbe wa kikao hiko kuhakikisha wanasimamia miradi iliyopo kwenye Kata zao huku aliwasisitiza Wakuu wa Idara na Vitengo kuwahusisha wajumbe hao na Wenyeviti wa Mitaa kwenye utekelezaji wa miradi kwenye maeneo yao.
Ameendelea kumsisitiza Mkurugenzi wa Manispaa mwalimu Hassan Nyange kutokubali kukatishwa tamaa badala yake aendelee kuchapa kazi kwa kuwa wananchi wanajua anachokifanya.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani amewaomba wajumbe wa kikao hiko kumpa ushirikiaano pale anapotimiza majukumu yake kwani yeye pamoja na Menejimenti yake imejipanga kuleta mabadiliko ndani ya Manispaa.
Katika kuhakikisha adhma yake inatimia kaunzia Januari 13, 2024 ataendesha Kampeni ya kuhakikisha wanafunzi wote waliaondikishwa kujiunga awali, darasa la kwanza wanakwenda shule na waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza wote wanaripoti.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.