Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mhe. Shadida Ndile, amesema hatua kubwa za kimaendeleo zilizofikiwa katika Wilaya ya Mtwara ni matunda yatokanayo na utawala bora na misingi imara ya uongozi iliowekwa na Viongozi wetu tangu tulipopata Uhuru.
Meya Ndile ameyasema hayo leo tarehe 9 Desemba, 2024 katika mdahalo maalumu kwa ajili ya kuadhimisha Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika kiwilaya katika Ukumbi wa Chuo cha Utumishi wa Umma-Mtwara.
Amesema ni vyema Wananchi hususani Vijana kuacha kubeza hatua hizo zilizofikiwa kiuchumi, kisiasa na kijamii na badala yake wazingatie historia na kujua ni wapi tumetoka ili kujua kiasi gani nchi yetu imepiga hatua kubwa.
"Tuwakumbushe vijana haya yote yanayoonekana na yanayoendelea kuonekana, na yote yaliyozungumzwa na wazee wetu leo yameundwa.... na usione vyaelea, vimeundwa," alisema.
Aliongeza kuwa lengo la kufanya mdahalo huo ni pamoja na kuwafundisha vijana na kuwarithisha historia nzuri ya nchi yetu ili iendelee kuwa na amani.
Aidha alitoa rai kwa vikundi vitakavyopata mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na Halmashauri kuitumia fursa hiyo kutumia kujikwamua kiuchumi.
Sambamba na hayo alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuwalinda watoto katika kipindi hiki cha likizo ili wawe salama na wasishiriki shughuli hatarishi huku akiwataka wazazi kuzingatia mila na desturi katika malezi.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.