Naibu Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wanawake na Watoto Dkt. Godwin Mollel amesema kuwa hospitali ya rufaa ya Kanda ya Kusini iliyopo Mitengo Manispaa ya Mtwara-Mikindani inatarajiwa kufunguliwa mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu.
Amesema kuwa ujenzi wa hospitali hiyo kwa sasa umefikia asilimia 97 na kwamba asilimia tatu zilizobaki zitakamilika hivi karibuni.
Dkt. Mollel ameyasema hayo Julai 26,2021 katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi katika hospitali hiyo iliyofanywa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango.
Ili kukamilisha jambo hilo Dkt. Mollel amesema kuwa Wizara imeomba kibali cha dharura cha kuajiri watumishi wapya 322 wa kada ya afya na itajumlisha watumishi 218 kutoka sehemu mbalimbali ili kufanya kazi katika Hospitali hiyo ya Kanda.
Ameongeza kuwa Serikali imetenga Bil. 6.5 kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba vitakavyotumika katika hospitali hiyo.
Ujenzi wa Hospitali ya rufaa Kanda ya Kusini umegharimu shilingi Bil. 15.8 na itahudumia Mikoa Mitatu ya Mtwara, Lindi na Ruvuma ikiwa na uwezo wa kulaza zaidi ya wagonjwa 900 kwa wakati mmoja.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.