Kutokana na usimamizi mzuri wa miradi ya Maendeleo inayotekelezwa ndani ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani imemvutia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo na kumpongeza Mkurugenzi wa Manispaa Col. Emanuel Mwaigobeko na timu yake kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo.
Jafo ametoa pongezi hizo Desemba 15,2020 alipofanya ziara ndani ya halmashuari na kufungua miradi miwili ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali kupitia mradi wa uendelezaji Miji Mkakati(TSCP) yenye gharama ya shilingi bilioni…….
Akizungumza mara baada ya Ufunguzi wa miradi hiyo Waziri Jafo ametoa rai kwa wananchi wa Manispaa kutunza miundombinu iliyojengwa ili iweze kudumu na kuwanufaisha vizazi vilivyopo na vijavyo.
Aidha jafo amewataka wawekezaji kuja kuwekeza Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa kuwa kwa sasa Manipaa hii ina miundombinu iliyobora ikiwemo miundombinu ya barabara na soko la kisasa la chuno.
Miradi iliyofunguliwa katika ziara hiyo ni Pamoja na mradi wa ujenzi wa soko la kisasa la chuno lililogharimu shilingi bilioni 5.3 na barabara ya COTC yenye urefu wa km 0.9 Iliyojengwa kwakiwango cha lami na kugharimu shilingi 1,709,742,321.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.