Jamii imetakiwa kuepuka na kuzipinga mila potofu zinazoathiri afya ya kinywa na meno kama vile kukata vimeo, meno dhaniwa ya plastiki na nyingine nyingi.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe. Abdallah Mwaipaya akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Col. Patrick Sawala, katika kilele cha maadhimisho ya kitaifa ya siku ya Afya ya kinywa na meno Duniani, Mkoa wa Mtwara yaliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa.
DC Mwaipaya pia amewaasa wanamtwara kuzingatia ushauri wa wataalamu wa afya kwa kufanya uchunguzi wa afya zao ili kubaini magonjwa katika hatua za awali na kuwezesha kupata matibabu stahiki kwa wakati ikiwemo yale ya kuziba meno.
Aidha, alisisitiza jamii kuepika matumizi ya sigara na bidhaa za tumbaku Pamoja na unywaji wa pombe uliopitiliza ili kuepuka na madhara kama vile magonjwa ya fizi, saratani kwenye ulimi, koo na kadhalika.
DC Mwaipaya ametumia jukwaa hilo kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha huduma na kuwekeza katika huduma za afya ya kinywa na meno.
“Katika Mkoa wetu wa Mtwara wenye jumla ya Halmashauri (9) jumla ya viti (Dental Chairs) 10, mashine 1 ya X – ray ya meno, na mashine 1 ya CT – Scan ya kinywa na meno zilinunuliwa, alisema.
Rais wa Chama Cha wataalamu wa Afya ya kinywa na meno Tanzania (TDA), Dkt. Gemma Zacharia, kwa upande wake alisema takribani watu bilioni 3.5 ulimwenguni huathirika na magonjwa ya kinywa na meno.
“Hapa nchini magonjwa ya fizi yanaathiri asilimia 62.8 ya watu wazima, na 57.4 ya Watoto. Tatizo la kuoza meno limeonekana katika jamii asilimia 31.1 ya Watoto”, alifafanua.
Kwa mujibu wake, siku ya afya ya kinywa na meno, iliasisiwa na shirikisho la afya ya kinywa na meno, duniani (FDI) Mwaka 2007 kwa lengo la uhamasishaji wa afya ya kinywa na meno Maaadhimisho hayo yalibebwa na kauli mbiu isemayo, “kinywa chenye furaha, ..iliyotafsiriwa toka kiingereza “A happy mouth is, ... a happy Mind.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.