Ujenzi wa jengo la kujifungulia Katika Zahanati ya Ufukoni umekamilika huku jengo hilo likitarajia kuhudumia akina mama zaidi ya mia mbili arobaini kwa mwezi waishio Kata ya Ufukoni na meneo mengine ya jirani.
Ujenzi wa jengo hili ambalo limegharimu shilingi milioni sabini na tanio (75,000,000) lina uwezo wa kuhudumia akina mama wanaojifungua wawili kwa wakati mmoja na kuhudumia akina mama wanaosubiri au wanaopata huduma baada ya kujifungua.
Kabla ya uwepo wa jengo hili Zahanati ya Ufukoni ilikuwa inatoa huduma ya upimaji na ushauri kwa akina mama wajawazito lakini ili kupata huma ya kujifungua iliwalazimu kutembea umbali wa kilomita zaidi ya tano kufuata huduma ya kituo cha afya Likombe au hospitali ya Rufaa ya Ligula.
Hivyo uwepo wa jengo la kujifungulia katika Zahanati hii inaenda kutatua Changamoto mbalimbali zikiwemo kupunguza idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi, kutembea umbali nmrefu kufuata huduma hii lakini pia kuwapunguzia gharama za usafiri.
Juni 4, 2021 Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI ilitoa shilingi Milioni Sabini na tano kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kujifungulia kwa akina mama , Lakini kutokana na usimamaizi mzuri wa Ofisi ya Mkurugenzi kwa kutumia fedha hizo hezo Zahanati imeweza kuongeza miundombinu mingine ikiwemo ujenzi wa kisima cha kuhifadhia maji ya mvua, mnara pamoja na tenki la kuhifadhi maji lenye ujazo wa lita 5000, ujenzi wa shimo la kuhifadhi kondo la uzazi (PLACENTA PIT) pamoja na ujenzi wa njia ya watembea kwa miguu (WALK WAY) inayounganisha jengo jipya na la zamani/
Manispaa ya Mtwara-Mikindani tunaishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kutuletea fedha zilizosaidia kuondoa changamotoza akina mama wajawazito Katika Manispaa yetu na sisi tunendelea kutoa huduma bora kwa akina mama hawa
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.