Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani kupitia ldara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imefanikiwa kuhimilisha jumla ya ng'ombe 253 kwa lengo la kupata ng'ombe wenye uwezo wa kuzalisha Maziwa mengi hivyo kumkwamua mfugaji kiuchumi.
Akiongea katika ziara ya kutembelea wafugaji waliopandisha Mifugo yao kupitia zoezi hilo la uhimilishaji wa Mifugo (Artificial Insermination - AI), Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Bw. Mipawa Majebele alisema zoezi hilo lilianza kutolewa Oktoba 2024 ambapo mpaka sasa Jumla ya ng'ombe 253 wamehimilishwa.
"Hapo awali huduma hii ilikuwa inatolewa na wataalam kutoka Wizara ya Mifugo hivyo ilipelekea wananchi kukosa huduma. Baada ya kuona upungufu wa ujuzi huo serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliwasomesha wataalamu wawili (2) katika kituo cha taifa uhimilishaji (NAIC) Arusha kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi," alifafanua.
Aliongeza kuwa, serikali pia ilitoa jumla ya dozi 100 za mbegu za ng'ombe za ruzuku, gesi ya Nitrogen lita 35 na dawa za vichocheo (Hormone) chupa 12 kwa lengo la kuhamasisha zaidi zoezi hili muhimu kwa wafugaji wa ngo'mbe.
Alisema lengo la huduma hii ni kuboresha mbari za Mifugo (BREED) na kuongeza uzalishaji wa Maziwa ambapo mfugaji anajiongezea kipato zaidi pamoja na kujipatia lishe yeye na familia inayowazunguka.
Akitoa mchanganuo wa huduma za upandishaji katika kata alisema Jumla ya kata 10 za Naliendele, Chuno, Likombe, Mtawanya, Magomeni, Tandika, Shangani, Ufukoni, Mitengo, na Mikindani wameshapandisha jumla ya ng'ombe 253.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.