Mkurugenzi wa Manispaa Mtwara-Mikindani aliyevaa trucksuit ya njano kulia akipokea mwenge w auhuru kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Omar Kipanga
Kutokana na utekelezaji mzuri wa miradi ya Maendeleo na usimamizi makini wa miradi umepelekea kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2018 ndugu Charles Francis Kabeho kuipongeza Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa kazi nzuri ya usimamizi wa miradi yenye viwango vya hali ya juu.
Pongezi hizo zimetolewa Juni 19 ,2018 wakati Manispaa ikikimbiza Mwenge wa Uhuru uliopitia jumla ya miradi 10 yenye thamani ya shilingi bilioni 4,6562,986,041 , Aidha pamoja na kupongeza usimamizi wa miradi ,pia kabeho ameipongeza manispaa kwa kuweza kutenga na kutumia fedha kutoka mapato yake ya ndani kwa utekelezi wa miradi 5 kati 10 iliyopitiwa.
Moja ya nyumba za zitakazokaliwa na wakuu wa idara
Wakati akitoa salamu za Mwenge wa Uhuru kiongozi huyo pia amewataka wazazi na walezi kuwapatia watoto chakula pindi wananpokuwa shuleni ili waweze kupata taaluma iliyobora na nzuri.
Aidha Kabeho amefafanua dhana ya uwekezaji katika elimu na kusema kuwa wanajamaii hao wana wajibu wa kuwekeza kwenye elimu kwa kujikusanya kufyatua tofali wenyewe na kujenga wenyewe au wanajamaii hao wanaweza wakachangishana fedha kwa ajili ya kujenga miundombinu kwa kuwa Serikali haijakataza jambo hilo.
Pamoja na kupitia miradi hiyo Kabeho amegawa pikipiki kwa watendaji wa Kata 5 kwa ajili ya kurahisisha utendaji wa kazi, amekabidhi hundi ya Tzs 122,100,000 kwa vikundi cha vijana na wanawake na mashine za ushonaji 10 kwa vijana, amekabidhi kadi za CHF kwa wazee na watoto waishio katika mazingiwa hatarishi pamoja na ugawaji wa vyandarua kwa akina mama waja wazito.
Pia amegawa zawadi kwa Walimu wa shule za Msingi na Sekondari masomo yao yaliyofanya vizuri kwenye mitihani ya Taifa iliyopita pamoja na zawadi kwa shule zilizoshinda kwenye usafi na zawadi kwa shule zilizoongoza kwenye mitihani yaTaifa ya mwaka jana, pamoja na ugawaji wa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike waishio kwenye mazingira magumu.
Mwenge wa Uhuru umepokelewa Manispaa ya Mtwara-Mikindani tarehe 19 June 2018 ukiwa na kauli mbiu unayosema “Elimu ni ufunguo wa Maisha wekeza sasa kw aMaendeleo ya Taifa letu”
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.