Watumishi waliopewa dhamana ya kuratibu na kusimamia mikopo ya 10% ya mapato ya ndani ya Halmashauri wameaswa kuwa weledi na kujiepusha na vitendo viovu iliwemo kuanzisha vikundi hewa.
Wito huo umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini, Mhe. Hassan Mtenga wakati akifunga mafunzo ya siku mbili kwa Maafisa Ugani, Watendaji kata na Mitaa, Polisi kata na baadhi ya wataalamu ngazi ya Halmashauri yenye lengo la kuwajengea uwezo kamati ya mikopo ngazi ya kata yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Chuo Cha Ualimu Mtwara Kawaida leo Oktoba 2,2024
Amesema Serikali haitafumbia macho mtumishi yeyote atakayeenda kinyume na malengo yaliyowekwa kwa ajili ya mikopo hiyo, hivyo watumishi wote wazingatie taratibu na kanuni zilizowekwa.
“Tufanye kazi kwa weledi, msiruhusu kupoteza ajira zenu kwa tamaa ya fedha” alisema Mhe. Mtenga.Sambamba na hilo, amewaasa wanasisa kuacha kuingilia shughuli za mfuko huo.
Awali Mkurugenzi wa Manispaa Mtwara-Mikindani, Mwalimu Hassan Nyange aliwataka watumishi hao kutoingia majaribuni na kubadili matumizi ya fedha hizo.
Aliwasisitiza kwenda kutumia mafunzo waliyoyapata kwenda kufanya kazi na kutimiza malengo ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anatamani Kila Mtanzania awe na maisha bora.
Naye Mwenyekiti wa huduma za jamii, Mussa Namtema, ambaye pia ni Diwani kata ya Chikongola aliwahusia watumishi hao kwenda kutumia mafunzo hayo kutenda haki kuratibu mikopo hiyo kwa ajili ya masl
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.